Bao la Medie Kagere: Simba SC 1-0 Azam FC (VPL – 23/10/2019)

Channel:
Subscribers:
2,640,000
Published on ● Video Link: https://www.youtube.com/watch?v=X8tF9rFAKaM



Duration: 1:38
126,979 views
462


Bao pekee la straika Mnyarwanda Medie Kagere limetosha kuipa Simba pointi tatu muhimu mbele ya matajiri wa Chamazi, Azam FC.

Ni katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, ukiifanya Simba kusalia kileleni ikiwa na pointi zake 15 baada ya kushinda mechi zake zote 5.

Azam FC yenyewe imepoteza mchezo wake wa kwanza baada ya kushinda mechi zote tatu zilizopita na hivyo kubaki kwenye nafasi ya sita na pointi tisa katika michezo minne.