MBEYA CITY 1-4 KAGERA SUGAR: HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (VPL - 24/10/2019)

Channel:
Subscribers:
2,640,000
Published on ● Video Link: https://www.youtube.com/watch?v=44oC-Mb5SDo



Duration: 32:07
4,811 views
25


Hali bado ni tete katika kikosi cha Mbeya City ambacho leo kikiwa nyumbani kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya kimekubali kipigo kinono cha mabao 4-1 kutoka kwa Kagera Sugar.

Magoli ya Kagera yamefungwa na Erick Kyaruzi dakika ya 18, Yusuph Mhilu dakika ya 28, Frank Ikobela dakika ya 32 na Geofrey Mwashiuya 61' huku goli la kufutia machozi la Mbeya City likifungwa na Mohamed Mussa dakika ya 36.

Mechi hiyo ya muendelezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara imeishuhudia Kagera Sugar ikiwa katika kiwango bora ambapo ushindi huo unawarejesha kwenye nafasi ya pili ya msimamo wa ligi huku wenyeji wao Mbeya City wakiporomoka hadi nafasi ya 19 na alama zao nne walizovuna katika mechi sita walizocheza.