HOTUBA YA RAIS MAGUFULI AKIWA BUTIAMA - 06/09/2018

Channel:
Subscribers:
2,630,000
Published on ● Video Link: https://www.youtube.com/watch?v=rY48pdsbkdE



Duration: 1:10:33
24,010 views
83


Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Septemba, 2018 ameendelea na ziara yake Mkoani Mara ambapo amezindua mradi wa ufugaji wa samaki kwa kutumia mabwawa na vizimba Mjini Musoma na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya lami ya Makutano – Natta (Sanzate).

Akiwa Butiama Mhe. Rais Magufuli ameongozana na Mke wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya lami ya Makutano - Natta (Sanzate) yenye urefu wa kilometa 50 na ambayo ujenzi wake utagharimu shilingi Bilioni 54.6.

Akizungumza na wananchi wa Butiama katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mwenge Kijijini Butiama Rais Magufuli amewahakikishia wananchi hao kuwa pamoja na kujenga barabara hiyo Serikali itaendelea kujenga barabara nyingine za kuunganisha Butiama, Mugumu na Tarime ili kuimarisha mawasilino na kuipa heshima Butiama na Mkoa mzima wa Mara ambako ndiko alikozaliwa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Rais Magufuli amemshukuru Mama Maria Nyerere na familia yote kwa mchango mkubwa uliotolewa na Hayati Baba wa Taifa katika kupigania uhuru, kujenga Taifa, kupigania ukombozi wa Mataifa mengi ya Afrika na kuipatia Tanzania heshima kubwa duniani, na ameahidi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itahakikisha tatizo la maji lililopo Butiama linatatuliwa haraka iwezekanavyo.

“Nakupongeza Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa kwa kuwa na mpango wa kuleta maji Butiama, nitafuatilia, haiwezekani mahali alipozaliwa Baba wa Taifa pakakosa maji, na wewe Waziri wa TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo hakikisha hospitali ya Butiama inaboreshwa haraka na nimeagiza ile shule ya msingi Mwisenge pale Musoma Mjini aliyosoma Baba wa Taifa inajengewa uzio na majengo yake yanaboreshwa” amesisitiza Rais Magufuli.




Other Videos By Azam TV


2018-09-07MAGAZETI: Magufuli, Tundu Lissu, Taifa Stars 'watawala' magazeti
2018-09-07Magufuli aipongeza JWTZ kwa ufugaji samaki
2018-09-07KIPYENGA CHA MWISHO: Je, penati ya Yanga SC vMtibwa ilikuwa na utata?
2018-09-06HABARI - AZAM TV 6/9/2018
2018-09-06MSHIKEMSHIKE VIWANJANI - AZAM TV 6/9/2018
2018-09-06Wanaume kwenda Sokoni Zanzibar....ni mapenzi au utamaduni?
2018-09-06Je, matumizi ya vipaza sauti vya wamachinga ni hatari iliyojificha?
2018-09-06TMA yatahadharisha menejimenti za maafa kujipanga kupunguza maafa
2018-09-06Makonda akagua miradi ya ujenzi wa miundombinu Dar es Salaam
2018-09-06Xi Jinping aipa Tanzania Bil. 90
2018-09-06HOTUBA YA RAIS MAGUFULI AKIWA BUTIAMA - 06/09/2018
2018-09-06Mwalimu afariki dunia akisimamia mitihani ya darasa la saba
2018-09-06Mashabiki wa soka Musoma ‘wazikataa’ Simba na Yanga (MAKALA - TPL 2018/19)
2018-09-06Lipuli FC: Lengo letu msimu huu ni nafasi tatu za juu (MAKALA - TPL 2018/19)
2018-09-06Tulifukia mbuzi katikati ya uwanja – Mchezaji wa zamani Singida United (MAKALA - TPL 2018/19)
2018-09-06Jerry Tegete ‘akiwakaanga’ wachezaji wenzake wa Kagera Sugar (MAKALA - TPL 2018/19)
2018-09-06Jaffo 'atema cheche' ubadhirifu wa bilioni 2 Nyang'hwale
2018-09-06Juma Nyosso: Niliwahi kusimamishwa mara mbili bila kujua kosa langu (MAKALA - TPL 2018/19)
2018-09-06Akamatwa kwa kuanzisha kiwanda cha kutengeneza na kuuza silaha
2018-09-06Wananchi walia na harufu kali kutoka kiwanda cha maziwa
2018-09-06Mabua ya mahindi yawa ‘lulu’ Kilimanjaro



Tags:
Magufuli
Butiama
ziara
Rais Magufuli
Mama Maria
Nyerere
Mwalimu Nyerere
mke
mama
wake
kiongozi
mkutano wa hadhara
Musoma
Azam TV
Nyerere Gorge
Gorge
Stieglier’s Gorge
Stiegler
HOTUBA
Hotuba ya Rais
Butiama musoma
Magufuli Butiama