Lipuli FC: Lengo letu msimu huu ni nafasi tatu za juu (MAKALA - TPL 2018/19)

Channel:
Subscribers:
2,640,000
Published on ● Video Link: https://www.youtube.com/watch?v=6-qoK4RDPL4



Duration: 18:48
637 views
3


Uongozi wa timu ya Lipuli FC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kupitia kwa Mwenyekiti wake Ramadhan Mahano amesema lengo kuu la timu hiyo msimu huu ni kumaliza ligi tukiwa kati ya nafasi tatu za juu.

Mahano ametoa kauli hiyo kwenye makala hii ambayo imefanya mahojiano na wadau mbalimbali wa timu hiyo, wakizungumzia maandalizi ya Lipuli FC kwenye Ligi Kuu msimu huu wa 2018/19.

Baadhi ya wachezaji waliozungumza kwenye Makala hii ni Ally Mtoni, Paul Nonga, Abdallah Makangana na Novalt Lufunga.
Naye kocha wa timu hiyo Selemani Matola amejinasibu kuwa msimu ana kikosi kipana. Matola pia amezungumzia ratiba ya ligi msimu huu. Matola pia ametoa tathmini yake juu ya usiriki wa timu hiyo msimu uliopita wa ligi.

Mwingine aliyezungumza kwenye Makala hii ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela ambaye amzungumzia soka la wilaya ya Iringa kiujumla.
Nao baadhi ya mashabiki wa soka mjini Iringa wakiwemo Geofrey Makeo, Ibrahim Shirima,.

Ritha Kabati ni mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa, naye mdau wa timu hiyo, ameeleza mikakati waliyonayo kama wabunge wa mkoa wa huo kuhakikisha timu yao inafika tatu bora.
Naye Mkuu mpya wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi amezungumza akiweka wazi malengo na matarajio ya watu wa Iringa juu ya timu hiyo.

Msemo wanaoutumia msimu huu ni “Sisi Lipuli tunabadili mchezo”







Tags:
Lipuli FC
Matola
Hapi
Iringa
Lipuli
wachezaji
michezo
ligi
Ligi Kuu Tanzania Bara
Azam TV
soka
Azam Sports
Philip Cyprian
Tanzania Premier League
ligi kuu
makala