Mechi ya Uganda vs Taifa Stars yachambuliwa, makocha, mashabiki watoa ya moyoni

Channel:
Subscribers:
2,640,000
Published on ● Video Link: https://www.youtube.com/watch?v=wNQuYVoazSM



Duration: 9:14
11,516 views
22


Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars jioni ya leo imetoka suluhu na Uganda katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON mwaka 2019.

Mara bada ya mchezo huo mashabiki wa timu zote mbili wamezungumza na Azam TV ambapo wale wa Uganda wameonesha kutofurahishwa na matokeo wakati mashabiki wa Tanzania wakifurahi na kuonsha kuridhishwa na kiwango cha timu yao.

Pia makocha wa timu zote mbili wamezungumza ambapo wote wameonesha kuridhishwa na mchezo huku Kocha wa Taifa Stars akiwapongeza wachezaji wake kwa kupambana kama alivyowaagiza na kufanikisha lengo la kutopoteza mchezo.

Jijini Dar es Salaam, mashabiki wameitazama mechi hiyo kupitia ZBC2 LIVE kwenye ‘Big Screen’ ndani ya dimba la Taifa, na wametoa maoni yao kwa jinsi walivyouona mchezo.

Je, suala la nidhamu kwenye timu linalosimamiwa na kocha, limekuwa na manufaa yoyote kwa Taifa Stars kwenye mchezo wa leo? Mchambuzi Ally Mayay anasema ‘NDIYO’ na ataja sababu hapa humu huku akiuchambua mchezo wenyewe. Je, wewe unasemaje?







Tags:
Mshikemshike
Taifa Stars
Uganda
Uganda vs Tanzania
Ally Mayay
uchambuzi
kufuzu
AFCON
CAF
soka
Tanzania