HOTUBA KAMILI YA RAIS MAGUFULI AKIWA MUSOMA - 05/09/2018

Channel:
Subscribers:
2,640,000
Published on ● Video Link: https://www.youtube.com/watch?v=IeeHmqmNUcc



Duration: 1:08:30
57,664 views
204


Rais Magufuli leo tarehe 05 Septemba, 2018 ameendelea na ziara yake katika mkoa wa Mara ambapo amezindua mradi wa maji safi na usafi wa mazingira wa Manispaa ya Musoma, kufungua barabara ya Simiyu/Mara – Musoma na kisha kuhutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja Mukendo Musoma Mjini.

Katika hotuba yake Rais Magufuli ameelezea kutoridhishwa na hatua zinazochukuliwa na viongozi wa Wizara, Mkoa wa Mara na vyombo vya dola dhidi ya mfanyabiashara Nyakilang’ani ambaye amelalamikiwa na wananchi wa Mwisenge katika Manispaa ya Musoma kuwa baada ya kuuziwa hoteli ya Musoma amezuia wananchi kukatiza katika eneo hilo wanapotaka kwenda katika mwambao wa ziwa Victoria na hivyo kulazimika kuzunguka umbali mrefu.

“Hoteli hii imechukuliwa tangu miaka 10 iliyopita, haijaendelezwa, wananchi wanakosa ajira, Serikali inakosa mapato halafu viongozi mpo mnamuangalia tu, huyohuyo Nyakilang’ani amepewa mradi wa maji wa mji wa Bunda huu mwaka wa 8 na mpaka sasa hautoi maji, viongozi mpo hamchukui hatua.

“Sasa nataka hoteli ya Musoma iliyojengwa na Baba wa Taifa kwa nia yake njema ya kuiendeleza Musoma ichukuliwe kwa sababu ameshindwa kuiendeleza” amesisitiza Rais Magufuli.

Rais Magufuli pia amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Mara kuwa Serikali itahakikisha inaujenga kwa kiwango cha lami uwanja wa ndege wa Musoma ili uweze kupokea ndege kubwa na ndogo, na kukamilisha ujenzi wa hospitali ya Musoma haraka ili ifanane na hadhi ya hospitali iliyopo katika Mkoa aliozaliwa Baba wa Taifa.




Other Videos By Azam TV


2018-09-05MSHIKEMSHIKE VIWANJANI - AZAM TV 5/9/2018
2018-09-05Muswada wa bodi ya taaluma ya walimu 'wavuruga' wabunge
2018-09-05Ekolojia ya wanyama hatarini kutokana na viumbe vamizi
2018-09-05Bei ya Petroli na Dizeli zashuka kwa baadhi ya mikoa, ufafanuzi watolewa
2018-09-05Naibu Spika 'agoma' kusoma barua ya Museveni kuhusu usalama wa wabunge
2018-09-05Mbwana Samatta: Tusitazame Uganda kama mechi kubwa, tulenge AFCON
2018-09-05Rais Magufuli aahidi kufukuza watu mradi wa maji mkoani Mara ukikwama
2018-09-05Balozi Kijazi ataka majina ya ufisadi tenda za wahandisi
2018-09-05Madiwani wa CUF waliosimamishwa kwa zaidi ya mwaka mmoja warejeshwa
2018-09-05Mahujaji 120 wa Tanzania warejea salama
2018-09-05HOTUBA KAMILI YA RAIS MAGUFULI AKIWA MUSOMA - 05/09/2018
2018-09-05Fumo Felician: Wachezaji wengi siku hizi hawajitambui (MAKALA - TPL 2018/19)
2018-09-05Wachezaji wa zamani Coastal Union wasimulia walivyoipigania timu hiyo (MAKALA - TPL 2018/19)
2018-09-05Nataka Mbao FC imalize ligi ikiwa nafasi nne za juu – Kocha Amri Said; (MAKALA - TPL 2018/19)
2018-09-05Siangalii uwezo wa mchezaji, naangalia nidhamu - Kocha wa Mwadui FC (MAKALA - TPL 2018/19)
2018-09-05JKT Tanzania: Mashabiki wengi watazihama timu zao na kujiunga na sisi (MAKALA - TPL 2018/19)
2018-09-05Magufuli atolea uvivu 'uwekezaji katika Musoma Hotel'
2018-09-05Simba na Yanga 'kukitifua' mechi za kirafiki Septemba 8 na Septemba 9 mwaka huu
2018-09-05Ummy Mwalimu 'kula sahani moja' na wanaopotosha kwenya mitandao ya kijamii
2018-09-05Simiyu yaja na mikakati ya kumkomboa mkulima wa Pamba
2018-09-05Zaidi ya shilingi bilioni 660 kujenga barabara za Dar es Salaam



Tags:
Magufuli
Rais
hotuba
Musoma
ziara
JPM
magufuli ziarani
ziarani musoma
CCM
Azam TV
Azam TWO