YANGA TV: Uongozi wa Yanga watoa kauli sakata la kiungo wake kufungiwa na FIFA (Ep. 13)

Channel:
Subscribers:
2,630,000
Published on ● Video Link: https://www.youtube.com/watch?v=grdssWjpXGI



Duration: 23:07
7,606 views
36


Baada ya kuwepo kwa taarifa za kufungiwa na FIFA kwa kiungo wa Yanga Mohamed Issa Banka, kwenye kipindi hiki uongozi wa klabu hiyo kwa mara ya kwanza umetoa kauli.

Kwenye kipindi hiki, uongozi wa klabu ya Yanga umeanza kwa kutoa taarifa kuhusu michango iliyokwishatolewa hadi sasa kupitia kampeni maalam ya kuichangia klabu inayoendelea. Kiasi kilichopatikana kwa mwezi Agosti mwaka huu kimewekwa hadharani Kaimu Katibu Mkuu wake Omary Kaaya.

Naye Afisa Habari wa timu hiyo Dismas Ten amezungumzia sababu za Yanga kuahirisha mchezo wao wa kirafiki uliokuwa umepangwa kupigwa Septemba 5 mjini Kigoma dhidi ya Singida United.

Dismas Ten pia amezungumzia maandalizi ya Yanga kuelekea mchezo wao wa Septemba 9 dhidi ya African Lyon ambao ni maalum kwaajili ya kulinda tembo.


Kipindi hiki pia kinakuletea meneja mpya wa timu ya wanawake ya Yanga, ‘Yanga Princes’ ambaye ni Zameda Mageka pamoja na Kit Manager Salma Makweta.

Mahojiano maalum na Nahodha wa Yanga Princes Frola Kayanda pia yanapatikana humu.

Kama kawaida, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ ameendelea kufanya uchambuzi wa mwendendo wa timu dimbani, na safari anazungumzia jinsi timu hiyo ilivyoanza ligi msimu huu.

Kipindi hiki kimeruka Ijumaa na tarehe 07/09/2018.







Tags:
Yanga TV
Yanga
MO Banka
Mohamed Issa
Yanga SC
Azam TV
michezo
Kaaya
Ten
Dismas
Azam Sports
Banka