MSHIKEMSHIKE VIWANJANI AZAM TV 7/9/2018

Channel:
Subscribers:
2,640,000
Published on ● Video Link: https://www.youtube.com/watch?v=WZ9tnKe_QKk



Duration: 17:21
2,276 views
14


Msemaji wa Klabu ya Simba Haji Manara awataka mashabiki wa timu hiyo kuiunga mkono timu ya Taifa Stars kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Uganda The Cranes mechi ya kufuzu Kombe la Afrika AFCON. Na kusahau kuhusu wachezaji wa timu yao kutemwa kwenye kikosi cha timu hiyo ya taifa,
Klabu ya soka ya Yanga imesema inaungana na Watanzania wote kuitakia ushindi Taifa Stars katika mchezo wake wa kesho Jumamosi dhidi ya Uganda wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika.

Klabu ya soka ya African Lyon ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, nayo haikuwa nyuma katika kuitakia kheri Taifa Stars kwani mkurugenzi wake, Rahim Zamunda amesema uzalendo ni muhimu kwa kila Mtanzania.

Watanzania na wadau wa michezo nchini wameombwa kuisaidia kwa hali na mali timu ya taifa Tanzania ya soka la ufukweni ili ifanye maandalizi ya kutosha kujiandaa na fainali za mataifa ya Afrika AFCON zitakazofanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini Misri.







Tags:
Azam TV
Azam TWO
Azam TV Habari
Habari
Simba
Haji Manara
Uganda The Cranes
Kombe la Afrika AFCON
Yanga
Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara
Rahim Zamunda
Taifa Stars
Hashim Ibwe